Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa hawza Iran, katika kulaani kitendo kinachofanywa na utawala wa Kizayuni waporaji kwa kuvamia kikamilifu Ghaza, alitoa tamko.
Sehemu ya tamko hilo amesema kwamba: Tunazitaka serikali zote, mataifa yote, wanazuoni, wasomi, taasisi za kisheria na mashirika ya kimataifa kulaani uvamizi wa kikamilifu wa Ghaza na kuitangaza kuwa ni haramu kisheria na batili.
Maandishi ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم
الحمد لله رب العالمین، و الصلاة و السلام علی سید الأنبیاء و المرسلین محمد و آله الطاهرین، و صحبه المنتجبین
Enyi umma wa Kiislamu, mataifa huru na watu wote wenye kufikiri kwa uhuru duniani!
Leo tumesimama mbele ya mojawapo ya jinai za kinyama na za kihaini zaidi katika historia ya kisasa; utawala wa Kizayuni waporaji na wavamizi, kwa msaada wa dhahiri wa nguvu za mabeberu, unakusudia kuivamia kikamilifu Ghaza, kuangamiza kabisa taifa imara la Palestina na kufuta kabisa utambulisho na uwepo wao kutoka katika ramani ya kijiografia ya historia yao. Kitendo hiki si tu ni uvamizi wa wazi wa ardhi na mauaji ya halaiki yaliyopangwa, bali pia ni uvunjaji wa wazi wa vigezo vyote vya kisheria, kibinadamu na kisharia kwa kiwango cha dunia nzima.
Kwa mujibu wa misingi isiyobadilika ya fiqhi ya Kiislamu, kuilinda ardhi iliyovamiwa na kuunga mkono taifa lililo dhulumiwa la Palestina ni jukumu la kisheria, la kimungu na wajibu wa dharura juu ya mabega ya Waislamu wote na watu wote huru duniani. Qur’ani Tukufu inasema:
وَ ما لَكُمْ لا تُقاتِلُونَ في سَبیلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفينَ مِنَ الرِّجالِ وَالنِّساءِ وَالْوِلْدانِ
Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto.
[Surah An-Nisāʾ: 75]
Kutokana na mtazamo wa sheria za kimataifa za umma, hatua ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni ni uvunjaji wa wazi wa Katiba ya Umoja wa Mataifa, hususan kanuni ya kuzuia matumizi ya nguvu, Mkataba wa Nne wa Geneva unaohusu ulinzi wa raia katika vita, na pia maazimio mengi ya Baraza la Usalama na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na Palestina, jinai hizi, kwa mujibu wa Mkataba wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (Roma), ni mfano dhahiri wa jinai za kivita, jinai dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki.
Tunazihimiza serikali zote, mataifa yote, wanazuoni, wasomi, taasisi za kisheria na mashirika ya kimataifa kwamba:
1. Kulaani uvamizi wa kikamilifu wa Ghaza na kutangaza kuwa ni haramu kisheria na batili.
2. Kutumia vyombo vyote vya kisheria, kisiasa, kiuchumi na hata vizuizi halali ili kusimamisha uvamizi.
3. Kufungua njia za kupeleka msaada wa dharura wa kibinadamu, chakula na dawa kwa watu wa Ghaza bila sharti lolote.
4. Kuwafikisha viongozi wa utawala wa Kizayuni mbele ya vyombo vya mahakama vya kimataifa kama wahalifu wa kivita.
Hawza, kwa kutegemea fiqhi ya muqāwamah na kwa mujibu wa mafundisho ya madhehebu ya Ahlul-Bayt (as), sambamba na kutangaza mshikamano kamili na taifa shujaa la Palestina, vinathibitisha kwamba mapambano yataendelea hadi kuikomboa kikamilifu ardhi ya Palestina, Quds Tukufu na sehemu zote takatifu za Kiislamu na Kikristo.
Tambueni kwamba wavamizi watashindwa mbele ya irada ya mataifa yenye kusimama imara na ahadi isiyoweza kukiukwa ya Mwenyezi Mungu:
إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا، وَ أَكِيدُ كَيْدًا، فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا
Hakika wao wanapanga mpango, Na Mimi napanga mpango, Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.
(Aṭ-Ṭāriq/15–17)
والسلام علی جمیع عباد الله الصالحین
Alireza A‘rafi
Mkurugenzi wa hawza Iran.
Maoni yako